Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Ardabil, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hassan Ameli, mwakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi katika mkoa wa Ardabil, katika hotuba za Swala ya Ijumaa za wiki hii zilizofanyika katika Msikiti wa Musalla wa Ardabil, mbele ya wananchi kutoka makundi mbalimbali, ametaja baadhi ya Aya za Qur'ani Tukufu zinazohusiana na ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kulipiza kisasi dhidi ya wahalifu na madhalimu, akasema: Mwenyezi Mungu ametoa ahadi ndani ya Qur'ani kwa kusema:
«إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِینَ مُنْتَقِمُونَ»
“Hakika Sisi tutalipiza kisasi dhidi ya wahalifu.”
Na katika kueleza mwenendo na kanuni za uumbaji, amesema:
«فَلَمَّا آسَفُونَا انْتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَاهُمْ أَجْمَعِینَ»
“Walipotukasirisha, tuliwalipizia kisasi, kisha tukawaghariki wote.”
Vilevile, amesema:
«وَعْدَ اللَّهِ حَقًّا ۚ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّهِ قِیلًا»
“Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo ya kweli, na ni nani aliye mkweli zaidi kuliko Mwenyezi Mungu katika kauli yake?”
Pia amesema:
«وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّهِ حَدِیثًا»
“Na ni nani aliye mkweli zaidi kuliko Mwenyezi Mungu katika maneno yake?”
Ameongeza kuwa uchaguzi wa Marekani na kuanguka kwa Trump kwa namna ya fedheha na udhalilifu ni sehemu ya kisasi cha Mwenyezi Mungu na kisasi cha aliyedhulumiwa dhidi ya dhalimu.
Amesema kuwa; kila siku ambayo uwezo na nguvu za Mwenyezi Mungu za kuangamiza madhalimu zinapodhihirika, kwa istilahi ya Qur'ani huitwa Yawmullah (Siku ya Mwenyezi Mungu).
Katika vita hivi, mara nyingi sana miujiza ya Mwenyezi Mungu na uwezo Wake wa kuangamiza madhalimu umejidhihirisha. Amesema kuwa; pande zote mbili za kisiasa nchini Marekani zinafanana kabisa, ni kama vipande viwili vya kitambaa kimoja, au makali mawili ya mkasi mmoja, huku mkasi huo ukiwa mikononi mwa Uzayuni wa kimataifa.
Amefafanua kuwa; udhalilifu na fedheha iliyompata dhalimu aliyetoa amri ya kuuawa kwa Kiongozi wetu, watoto wa Minab na Kamanda Suleimani, kisha akajivunia kitendo hicho, na kusababisha kuuawa kishahidi maelfu ya wananchi wetu, pamoja na Netanyahu ambaye kwa kutegemea uungwaji mkono wake aliwaua Wapalestina 80,000 wasio na hatia, ni ushindi mkubwa mno kwa Jihadi ya Haki na Jihadi ya Muqawama.
Amesema kuwa; jambo hilo linaonesha kwamba Mwenyezi Mungu si mtazamaji tu, wala hajaghafilika na jinai zinazofanywa na watawala wanaotenda mambo kwa matakwa yao binafsi.
Mwenyezi Mungu anasema:
«وَلَا تَحْسَبَنَّ اللَّهَ غَافِلًا عَمَّا یَعْمَلُ الظَّالِمُونَ»
“Wala usidhani kwamba Mwenyezi Mungu amegafilika na yale wanayoyatenda madhalimu.”
Na amesema:
«وَمَا كَانَ رَبُّکَ نَسِیًّا»
“Na Mola wako si mwenye kusahau kamwe.”
Vilevile, Amirul-Muuminina Imam Ali (a.s) amesema kuwa siku ya aliyedhulumiwa ni kali zaidi kuliko siku ya dhalimu.
Ameeleza kuwa Mwenyezi Mungu anauendesha ulimwengu huu kwa mujibu wa kanuni maalumu, miongoni mwa malaika wanaotekeleza mipango ya Mwenyezi Mungu ni wale wanaosimamia mambo kwa amri Yake (Wal-Mudabbirati Amran).
Miongoni mwa kanuni za uumbaji ni kauli isemayo:
«مَنْ أَبْکَی النَّاسَ ظُلْمًا سَیُبْکِیهِ الزَّمَانُ قَهْرًا»
“Yeyote anayemsababishia mwanadamu mwingine kulia kutokana na dhuluma, basi zama zitamliza yeye mwenyewe kwa namna ya lazima.”
Amesisitiza kuwa; hii ni kanuni isiyoweza kuepukika, hata kama muda utakuwa mrefu, amesema kuwa haiwezekani kuufanyia mzaha uvumilivu wa Mwenyezi Mungu wala kuchezea subira Yake, katika historia, watu wengi waliuchukulia kirahisi uvumilivu na ghadhabu za Mwenyezi Mungu, lakini hatimaye waliona matokeo yake.
Ameongeza kuwa; Carter wakati wa shambulio dhidi ya Iran, alisema: “Kila kitu kilikuwa upande wetu, lakini Mwenyezi Mungu alikuwa pamoja na Iran.”
Kushindwa kwa Trump lilikuwa jambo lililotabirika
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Ameli, katika kuendelea na mazungumzo yake, akisisitiza kuwa kushindwa Trump kulikuwa jambo lililotabirika, amesema:
Trump ndiye rais mwenye kiburi zaidi, majivuno makubwa zaidi, udanganyifu mkubwa zaidi wa nafsi, ujinga mkubwa zaidi na kujipenda kupita kiasi katika historia ya Marekani. Tabia hizi mbaya zenyewe zinatosha kumwangusha mwanadamu, kwa hiyo, kuanguka kwake kwa fedheha na udhalilifu lilikuwa jambo lililotabirika kabisa.
Ameongeza kuwa; Mwenyezi Mungu alimshusha kutoka kileleni hadi kwenye hali ya chini kabisa, na bila shaka, kwa mujibu wa kanuni za uumbaji, atazidi kudhalilika na kufedheheka zaidi ya hapo, machozi ya mtu aliyedhulumiwa katika ulimwengu huu hayapotei bure kamwe.
Amesema: Hata kama tungetumia mabilioni ya dola, tusingeweza kupata matokeo haya dhidi ya adui yetu. Katika riwaya imeelezwa kuwa; Mwenyezi Mungu anapotaka kumwadhibu mtu, humwondolea uwezo wake wa kutumia akili, kisha mtu huyo hufanya kosa kubwa, baadaye Mwenyezi Mungu humrudishia akili yake, na hapo huanza kujilaumu na kujiuliza: Ni kosa gani kubwa kiasi hiki nililolifanya?
Kosa la Trump lilikuwa ni kuidharau Iran na wananchi wa Iran.
Ameeleza kuwa; Trump amekiri kwamba sababu ya kushindwa kwake ni vita dhidi ya Iran. Kwa hiyo, baada ya kushindwa anaweza kuchukua mojawapo ya maamuzi mawili:
La kwanza, kusema kwamba ni lazima tusitishe haraka vita hivi vya maafa ili tujiokoe na madhara makubwa zaidi yatokanayo navyo.
La pili, kutaka kulipiza kisasi dhidi ya Iran na kufanya jinai mpya.
Amesema kuwa; taarifa zilizotolewa kutoka Ikulu ya White House zinaonesha kuwa chaguo la kwanza ndilo linaloelekea kufuatwa. Trump anafanya mashauriano na washauri wake wakuu kuhusu namna ya kumaliza vita hivi haraka iwezekanavyo. Ameongeza kuwa iwapo Trump ana akili, bila shaka atachagua njia ya kwanza.
Kisha amenukuu methali yenye hekima isemayo:
«الْعَاقِلُ یُغَیِّرُ رَأْیَهُ إِذَا ظَهَرَتْ لَهُ الْحَقِیقَةُ، أَمَّا الْجَاهِلُ یُغَیِّرُ الْحَقِیقَةَ إِذَا خَالَفَتْ رَأْیَهُ!»
“Mwenye akili hubadilisha msimamo wake pale ukweli unapodhihirika kwake, ama mjinga, hujaribu kuubadilisha ukweli pale unapokuwa kinyume na maoni yake!”
Hakuna uwezekano wa Marekani kufanya shambulio jingine dhidi ya Iran
Imam wa Swala ya Ijumaa wa Darul-Irshad, akizungumzia kutokuwepo kwa uwezekano wa Marekani kufanya shambulio jingine dhidi ya Iran, amesema: Moja ya sababu zinazofanya uwezekano wa shambulio jingine kuondolewa ni kwamba Wamarekani hawawezi kubainisha lengo la vita au shambulio jipya.
Iwapo lengo lao ni kuangamiza sekta ya nyuklia ya Iran, hilo haliwezi kutimizwa kwa kufanya mashambulizi, iwapo lengo ni kufungua Mlango-Bahari wa Hormuz, hilo pia haliwezi kutatuliwa kwa mashambulizi, na iwapo lengo ni kuipindua serikali ya Iran, basi hilo linahitaji mashambulizi ya ardhini, katika hali hiyo bila shaka wanajeshi wa Marekani wataangamizwa kwa wingi.
Kwa upande mwingine, taifa ambalo limeamka na kuhamasika, na ambalo wananchi wake wanajitokeza mitaani kila usiku, halitatoa nafasi ya kufanyiwa mashambulizi dhidi ya mfumo wa utawala.
Ameongeza kuwa jambo moja la kushangaza katika uchaguzi huu ni kwamba dunia nzima ilisherehekea kushindwa kwa Trump. Hili ni baya zaidi kuliko vifo elfu moja; ni jambo kubwa zaidi hata kuliko bomu la nyuklia, hii ni sehemu ya kisasi chetu.
Amesema kuwa; sababu kuu ya kisasi hiki ni Muqawama wa wananchi wetu na ushujaa wa vikosi vyetu vya ulinzi.
Ameeleza kuwa; pia tumepata kisasi kingine, nacho ni kwamba Trump amekumbwa na lawama, karipio na shutuma kali kutoka pande mbalimbali.
Kwanza, Republican wamemshambulia kwa lawama kali, wakimuuliza: Je, vita dhidi ya Iran vilikuwa na thamani ya kutufanya tupoteze viti vyetu katika Baraza la Congress, Seneti na nafasi za ugavana kwa miaka mingi? Je, vita dhidi ya Iran vilikuwa na thamani ya kutuvunjia heshima ndani na nje ya Marekani? Amesema kuwa kwa sasa Trump amejikuta katika hali nzito mno ya kuwajibika na kubeba lawama.
Pili, nchi za Ulaya na nchi zilizoendelea kiviwanda zimemuweka chini ya lawama kali, zikimuuliza kwa nini ameupooza na kuudhoofisha uchumi wao kwa kuishambulia Iran.
Tatu, nchi za Ghuba ya Uajemi zinamwambia: Katika kuishambulia Iran umeshindwa kufanya chochote, lakini umeharibu usalama na uchumi wetu.
Nne, lawama hizo zinatoka pia kwa AIPAC, yaani taasisi ya ushawishi ya Uzayuni wa kimataifa. Wanamwambia Trump kuwa; kutokana na mwenendo wake wananchi wa Marekani wamegeuka kuwa wapinzani wa Israel na Uzayuni.
Amesema kuwa lawama hii ndiyo inayomtisha Trump zaidi kuliko zote, kwa sababu AIPAC ndiyo yenye ushawishi mkubwa katika masuala ya fedha na propaganda za uchaguzi nchini Marekani. Trump amefanya uharibifu mkubwa kiasi kwamba hata AIPAC haikuweza tena kujionesha kwa nguvu katika uchaguzi wa hivi karibuni.
Uchaguzi wa Marekani ulikuwa ni ujumbe wa wananchi dhidi ya Israel
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Ameli amesema kuwa; uchaguzi huu ulikuwa ni namna ya Wamarekani kuionesha Israel hasira na chuki yao. Amefafanua kuwa; watu wote ambao hawakuwapigia kura Republican walifanya hivyo kutokana na vita dhidi ya Iran. Vita hivyo dhidi ya Iran vilikuwa vimeelekezwa kwa Trump na Israel.
Amesema kuwa; katika vita vya hivi karibuni, na hasa katika uchaguzi wa Marekani, Israel imepoteza ngome yake ya mwisho ndani ya Marekani. Jambo hili kwa kweli halijawahi kutokea katika historia.
Ameongeza kuwa wapiga kura wengi wa Democrats nchini Marekani walitangaza kwamba hawatampigia kura mgombea anayeungwa mkono na AIPAC. Amesema kuwa taasisi ya ushawishi ya Israel, ambayo hapo awali ilikuwa ikiwatishia kwa jeuri viongozi wa Marekani na kuipangia Marekani sera zake, kwa sasa haina tena nyenzo yoyote ya shinikizo mikononi mwake, na imepoteza kura zake katika majimbo yote.
Kabla ya uchaguzi, tafiti za maoni zilionesha kuwa asilimia 60 ya wapiga kura walisema hawatawahi kumpigia kura mgombea yeyote anayefadhiliwa na AIPAC, wala wale wanaoiunga mkono Israel. Ameongeza kuwa hata Trump mwenyewe anakiri jambo hili, akisema kuwa Schumer (mchambuzi mkubwa wa Marekani) anazungumza kana kwamba yeye mwenyewe ni Mpalestina.
Amesema kuwa; kwa miaka mingi Israel ilikuwa ni mstari mwekundu katika siasa za Marekani. Republican, Democrats, watu wa mrengo wa kushoto na wahafidhina wote walikuwa na kanuni moja waliyoichukulia kuwa takatifu, nayo ni kwamba hakuna mtu aliyepaswa kuikosoa au kuishambulia Israel. Lakini leo hii, mitaa yote ya Marekani imejaa maandamano yanayoipinga Israel.
Ameeleza kuwa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa na vita dhidi ya Iran vimebadilisha mtazamo wa wananchi wa Marekani, na kanuni hiyo iliyokuwa ikichukuliwa kuwa takatifu imevunjika kabisa. Hapo awali, ukosoaji wowote dhidi ya Israel ulipokuwa ukitolewa, ulifanyika kwa siri. Lakini hivi sasa ukosoaji huo unatolewa waziwazi, mchana kweupe, ndani ya Congress, katika vyuo vikuu, katika vituo vya utamaduni na hata miongoni mwa kizazi kipya cha Marekani. Kwa mara ya kwanza, Wamarekani wameonesha mshikamano na huruma zaidi kwa Wapalestina kuliko wanavyoonesha kwa Waisrael.
Maoni yako